Leo February 12, 2018 Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa bado wanasubiri nyaraka za kesi ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, inayomkabili mfanyabiashara , Ndama Hussein ‘Ndama mtoto ya Ng’ombe’ kutoka nchini Australia.
Hata hivyo, Ndama ameshindwa kufika Mahakamani hapo leo February 12,2018 kwa sababu anaumwa.
Wakili wa Serikali, Estazia Wilson, amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa, kuwa. wameshapeleka maombi, kwa ajili ya kupata nyaraka za kesi hiyo.
Hata hivyo Ndama hakuwepo Mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa. Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Nongwa, ameahirisha kesi hiyo hadi February 28, 2018 itakapotajwa.
Ndama anakabiliwa na mashtaka matano ambapo anadaiwa kuwa February 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye Kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
Pia anadaiwa March 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha Kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.
ALICHOZUNGUMZA KIBATALA BAADA YA SUGU KUACHIWA, AMETAJA KILICHOKUWA KINAKWAMISHA DHAMANA