Mara nyingi Wataalamu wa afya na Washauri mbalimbali wa ishu za saikolojia wamekuwa wakijaribu kueleza mambo yanayosababisha mtu kukosa usingizi huku pia wakieleza mbinu au namna ya kukufanya upate usingizi mzuri na kwa haraka.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CNN, zimetajwa njia sita za kufuatwa na mtu yeyote anaesumbuliwa na kukosa usingizi.
1: Kuvaa soksi wakati wa kulala
Kama ulikuwa hujui ni kwamba kuwa na miguu yenye joto kunaweza kukusaidia kupata usingizi, Watu wanashauriwa wakati wa kulala kuvaa soksi ili kupata usingizi kwa haraka kwa sababu soksi hutengeneza joto litakalokurahisishia usingizi.
2: Lala chumba chenye giza
Wataalam wanasema kuwa hata kiwango kidogo kabisa cha mwanga huweza kukuharibia usingizi wako hivyo wanashauri ili upate usingizi haraka na uweze kulala vizuri unatakiwa kuzima taa zote chumbani na pasiwe na mwanga.
3: Fanya mazoezi
Unaambiwa pia kuwa miongoni mwa mambo yatakayokufanya uufurahie usingizi wako ni kufanya mazoezi ambapo kwa mujibu wa Wataalamu ni kwamba hata dakika chache za kufanya mazoezi kwa siku zinaweza kuutengeneza vizuri usingizi wako.
4: Paka rangi zisizong’aa chumbani
Kupaka rangi za kung’aa chumbani ni moja ya sababu za kukuchelewesha kupata usingizi hivyo unashauriwa kupaka rangi ambazo haziakisi mwanga ili kukufanya upate usingizi wa haraka na raha.
5: Yoga
Yoga inaweza kukusaidia kujituliza na kutuliza akili yako, inatajwa pia kulegeza mfumo wa upumuaji na kurekebisha kasi ya mapigo ya moyo ili kuufanya usingizi wako uwe muruwa.
6: Ota kwenye jua la asubuhi
Kujianika kwenye jua la asubuhi kutakusaidia kuuamsha ubongo wako na kuufanya uwe tayari kwa ajili ya kazi za siku na kukusaidia kupata usingizi mapema wakati wa usiku.
Taarifa ya Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebola nchini. Bonyeza play hapa chini kutazama…
Wizara ya Afya imeomba kutengewa Bajeti ya Trilion 1.1…