Muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Tutubert Gama, Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge Job Ndugai huku akieleza kuwa marehemu alikua kiongozi hodari, aliyefanya kazi kwa kujiamini na aliyependa kupigania maslahi ya wananchi bila kuchoka.
Gama amefariki dunia jana November 23, saa 4:25 usiku katika hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho iliyopo Songea baada ya kukimbizwa huko kwa matibabu alipougua ghafla.
Ulipitwa na hii? “Nimekuteuwa juzi umeshaanza kufikiria Majengo, unanifanya nifikirie zaidi” – JPM