Fulham ni mmoja wa wafungaji wa chini zaidi katika Premier League msimu huu wakiwa na mabao 13 pekee, na gazeti la Daily Mail linaripoti kuwa watamlenga mshambuliaji wa Chelsea mnamo Januari.
Kocha wa Cottagers, Marco Silva amemtambua Armando Broja wa Chelsea kama mtu anayeweza kuponya matatizo yao ya upachikaji mabao.
Klabu hiyo ya London Magharibi ilishindwa kuchukua nafasi ya Aleksandar Mitrovic baada ya kuondoka kuelekea Saudi Arabia majira ya joto na wamekuwa wakilipa bei hiyo.
Broja hivi majuzi alirejea kutoka katika jeraha la muda mrefu na huenda akapatikana huku Chelsea ikitafuta wachezaji kabla ya kuleta sura mpya.
Fulham wanatumai kuwa Chelsea itamruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuondoka kwa mkopo kwa muda uliosalia wa msimu huu.