Mkosi wa mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la dunia umeendelea kutamba kwenye michuano hiyo.
Baada ya Ufaransa bingwa wa 1998 kutolewa raundi ya kwanza 2002, Italy bingwa wa 2006 kutolewa kwenye makundi 2010, leo hii historia hiyo imeendelea baada ya bingwa wa 2010, timu ya Taifa ya Spain maarufu kama La Roja kuaga mashindano hayo.
Wakicheza mechi yao ya pili dhidi ya Chile, La Roja wamevuliwa ubingwa kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chile.
Alikuwa Eduardo Vargas kwenye dakika ya 20 aliifungia Chile goli la kuongoza, lakini mchezaji CH. Aranguiz akafunga kazi kwa kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Spain.