Mechi za hatua ya 16 zimemalizika rasmi usiku wa kuamkia leo kwa mchezo kati ya Marekani dhidi ya Belgium.
Katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote, mpaka dakika zote 90 zinamalizika hakukuwa na mtu aliyefanikiwa kuliona lango la mwenzie, japo kulikuwa na kosa kosa nyingi katika lango la Marekani na bila ushujaa wa kipa Tim Howard basi hadithi ingekuwa nyingine.
Baada kwa kumalizika kwa dakika 90, zikaongezwa dakika 30 za nyongeza na mnamo dakika ya 105, Kelvin De Bruyne akaifungia Belgium bao la kwanza, dakika 2 baadae Romelu Lukaku akapiga goli la pili, kabla ya Green kuifungia Marekani goli la kufutia machozi.