Hekaheka ya leo inatokea Shinyanga ambapo wanafamilia pamoja na majirani walimzuia mke wa marehemu kwenda kumzika mume wake kwa madai kuwa alikuwa akimnyanyasa enzi za uhai wake.
Wakati mume wake anafariki mama huyo hakuwepo na alipopigiwa simu kuwa mume wake amefariki alirudi nyumbani na kuwakuta ndugu wa mume wake na majirani wakiomboleza lakini yeye aliwakasirisha watu kuonekana kama hakujali.
Majirani wanasema aliwahi kumkana mume wake tangu zamani pamoja na kumtesa huku akiishi na mume mwingine ambaye ni mume wa mtu, na walikuwa wakiishi ndani ya nyumba ya mume wake ambaye amefariki.
Ndugu wa mume wakashirikiana na majirani na Mwenyekiti wa mtaa, wakaamua kumshusha kwenye gari mama huyo na watoto wake ili wasiende kwenye mazishi Bukoba ambako mwili wa Marehemu ulipelekwa kwa ajili ya mazishi.
Hekaheka yote nimeirekodi na kukuwekea hapa mtu wangu…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.