Papa aliyasema hayo wakati wa katekesi iliyohusu “maovu ya tamaa” katika hadhira yake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro siku ya Jumatano.
“Furaha ya ngono ni zawadi kutoka kwa Mungu” lakini Wakatoliki wanapaswa kuepuka ponografia, Papa Francis amesema.
Raha ya ngono ilikuwa kitu cha kuthaminiwa, alisema, lakini ilikuwa “ikidhoofishwa na ponografia”, na “kuridhika bila uhusiano kunaweza kusababisha aina za uraibu”.
“Lazima tutetee upendo,” papa alisema.
Lakini aliongeza: “Kushinda vita vya tamaa kunaweza kuwa jambo la maisha yote.” Francis alionekana kuwajibu wakosoaji wake wa kihafidhina, ambao walikasirishwa wiki iliyopita baada ya kitabu kuibuka tena chenye maudhui ya ngono wazi yaliyoandikwa miongo kadhaa iliyopita na mkuu wa mafundisho wa Vatikani.
Mnamo 2022, wakati wa mazungumzo na wanasemina kuhusu hatari za mitandao ya kijamii, papa alionya dhidi ya “shetani” wa ponografia ya kidijitali, huku akikiri kwamba makasisi na watawa pia hutazama ponografia mtandaoni.
“Ni tabia mbaya ambayo watu wengi wanayo. Walei wengi sana, walei wengi sana, na pia makasisi na watawa,” alisema. “Ibilisi huingia kutoka huko.”