Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti September 16 2016 ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Anyofolewa ulimi’
#HabariLEO Kijana Singida anyofolewa kipande cha ulimi na mke wa jirani yake aliyemlazimisha kufanya naye mapenzi pic.twitter.com/o4KnnZGjQV
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
Kijana mkazi wa Unyakhae nje kidogo ya mji wa Singida, Said Mnyambi (26) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kunyofolewa kipande cha ulimi wake na mke wa jirani yake aliyekuwa anamlazimisha kufanya nae mapenzi.
Kwa mujibu ya maelezo ya kijana huyo, tukio hilo limetokea siku ya Idd El Haji Jumatatu wiki hii saa 3:30 usiiku.Alieleza kuwa siku ya tukio, mke wa jirani yao mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake, alimwomba amsindikize nyumbani kwa kuwa amelewa .
Alidai walipofika njiani,mama huyo alimtaka wafanye naye mapenzi jambo ambalo kijana huyo alimkatalia lakini alimwomba angalau waagane kwa kunyonyana ulimi (denda) naye akamkubalia.
‘Nilimkubalia kumpa denda na hapo ndipo alipoanza kufungua mkanda wa suruali yangu, lakini nilipomkatalia kufungua mkanda wangu hapo ndipo alipong’ang’ania ulimi wangu hadi akanyofoa kipande na yeye akakimbilia kwake’;- Said Mnyambi
Alipoulizwa iwapo mama huyo ni mpenzi wake, kijana huyo alikataa kata kata na kujitetea kuwa alimuomba amsindikize kwa vile tu anamfahamu na ni jirani yake.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dk Ramadhani Kabala alithibisha kunyofolewa kwa kipande cha ulimi wa kijana huyo na kueleza kuwa alifika hospitalini hapo kwa matibabu baada ya ulimi wake kupata maambukizi na kuingia usaha hadi kushindwa kuongea.
Unaweza kupitia habari zingine kwenye magazeti ya Tanzania
#NIPASHE Takwimu zilitotolewa na MOI zaonyesha kila siku majeruhi bodaboda mmoja huitaji kuwekewa kiungo cha bandia pic.twitter.com/0oJq7tYUlG
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#NIPASHE NIDA imesema kuna uwezekano mkubwa vitambulisho vya Taifa kutumika ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 pic.twitter.com/3CWrBrXIsq
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#NIPASHE Mil 85.58 zimepatikana baada ya wabunge kukatwa posho ya siku moja kuchangia waathirika wa tetemeko pic.twitter.com/cfFIe6LuLS
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#NIPASHE Twaweza imetoa ripoti inayochambua utendaji wa Rais Magufuli ambayo inaonyesha anakubalika kwa asilimia 96 pic.twitter.com/uOR3ZW6E2I
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Waasi Congo wachoma malori ya Tanzania, wataka kila dereva alipiwe mil 8.8 ili waachiwe huru pic.twitter.com/0VOwDNwjxk
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kuwa miongoni mwa sababu zitakazochelewesha mkutano wa Rais na viongozi wa dini kuhusu UKUTA pic.twitter.com/WZZAwHp9zu
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Spika Ndugai ametuma salamu NIDA, akiitaka kujiweka vizuri kwa kuwa sasa utawala umebadilika pic.twitter.com/DNnTFYsMfF
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Aliyehukumia miaka 60 Moshi kwa kumbaka na kumlawiti mwanaye ajiua kwa kunywa sumu akiwa mahabusu pic.twitter.com/u4xSlgQ2YU
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI TRA imewataka wamiliki wa vituo vya mafuta Arusha kutumia mashine za EFD la sivyo watavifunga pic.twitter.com/yDl5ccBfjH
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Wabunge wahoji Serikali kushindwa kuweka ukomo wa nauli ya ndege, abiria Dar-Mwanza kuendelea kuumia pic.twitter.com/WG2mOsEh4n
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Uwanja wa ndege Mwanza kuhudumia abiria mil 2 kwa mwaka kutoka 500,000 baada ya ujenzi wake kukamilika pic.twitter.com/qNdNIVqZdv
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
#MWANANCHI Imebainika mabaki ya ndege yaliyokutwa Pemba ni ya shirika la Malaysia Airlines iliyotoweka 2014 pic.twitter.com/LczAbIJDhg
— millardayo (@millardayo) September 16, 2016
ILIKOSA HII YA MTANZANIA ANAYEFANYA KAZI TAASISI YA BILL GATE, ALIWAHI KUWA WA MWISHO DARASANI? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI