Leo February 6, 2018 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukeketaji duniani, Shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa UN Women limefanya uteuzi.
Shirika hilo limemteua Mwanaharakati Jaha Dukureh wa nchini Gambia kuwa Balozi wa Ukarimu yaani Goodwill Ambassador wa bara la Afrika wa shirika hilo.
Dukureh atasaidia katika kufanya utetezi kwenye kutokomeza kabisa ukeketaji kwa wanawake (FGM) na ndoa za utotoni barani Afrika akiweka focus yake kubwa katika kuhamasisha vijana.
“Lazima tukomeshe ukeketaji na ndoa za utotoni, nataka kuona siku ambayo hakuna mzazi ambaye atafanya maamuzi yatakayobadilika na kukomesha maisha ya mabinti zao.” – Jaha Dukureh
Mbunge Malecela kuhusu wanaosema Serikali ya Magufuli haijafanya lolote
Kauli ya Prof Tibaijuka kuhusu Diwani CHADEMA aliyedaiwa kutekwa