Ni September 7, 2016 ambapo Meya wa Manispaa wa Ilala, Charles Kwiyeko alieleza juu ya ulipaji kodi kwa wafanyabishara wa manispaa yake pamoja na utekelezwaji wa Usafi.
Akizungumza hayo na Ayo TV & Millardayo.com alisema’Wamachinga wakili kwanza wao ndio watekeleza suala la usafi ambapo walikuwa na kikundi maalamu cha ulinzi shirikishi ambacho kinaangalia vitu vyao pamoja na biashara zao, sasa katika kero ya usafi tulikubaliana nao kwamba watahakikisha usafi utakuwepo katika Manispaa yangu’
‘Kodi ni umuhimu kwa kila mfanyabiashara tutahakikisha Kila mfanyabiashara anahusika katika ulipaji wa kodi kumekuwa na malalamiko juu ya wenye maduka ya jumla na wamachinga juu ya Risiti unakutana wamachinga wanaouza rejareja na hawa wa maduka wanauza jumla, kwahiyo tunaangalia namna ya kuweza kutatua hapo
Unaweza ukabonyeza play kuitazama hii video hapa
ULIKOSA MAJIBU YA WAZIRI NCHEMBA KWA MBOWE KUHUSU MADAI YA DENI LA TAIFA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA