Leo December 14, 2017 Rais John Magufuli amefungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mjini Dodoma. hizi ni kauli kubwa 10 alizozisema wakati akitoa hotuba yake
"Wakati tunapata Uhuru nchi yetu ilikuwa na shule za msingi 3100 lakini katika kipindi cha mika 57 ya Uhuru tumeweza kujenga shule za msingi 14279 na kufanya nchi yetu iwe na shule 17379. " – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Katika kipindi hicho tumekuwa na shule za sekondari zilikuwa 41 lakini sasa tuna shule za sekondari 4817, tulikuwa na chuo kikuu kimoja lakini leo tunavyo 48, bila shaka mtakubaliana nami kuwa haya ni mafanikio makubwa sana." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi za dhati kwa viongozi wa awamu mbalimbali za nchi yetu kwa kufanikisha kupatikana kwa mafanikio haya." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Yapo majengo mengi ambayo hayawezi yakaitwa shule wala chuo kama hayana walimu, yataitwa majina mengine. yanaweza yakaitwa hospitali au bar lakini panapokuwa na walimu majina yanabadilika." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Haya madeni ya walimu, kama ni ya halali nawahakikishia tutayalipa yote" – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Serikali mipango yake ni kuboresha maisha wa Watanzania wakiwemo walimu, nia ni kushughulikia mahitaji yote kwa ujumla, hivyo mnapoweka madai yenu mbele ni lazima pia mtambue uwezo wa nchi yetu." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Tulikuwa na madini yetu, nafikiri yangekusanywa vizuri tusingekuwa tunalia hivi, yameibiwa na nafikiri alikuwa anaibiwa mwehu, wamesomba kwa kiwango cha kupitiliza." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Kuna mtu alisema walimu wanaidai serikali Tril 1 na zaidi, na nikajaribu kuuliza fedha 2% zinazokatwa kwenye mishahara ya mwezi zinatumikaje?hakuna jibu, mnajua kuyadai ya serikali lakini yanayowahusu ninyi hamyajui kuyauliza." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Agizo langu la kutomuhamisha mwalimu mpaka atakapolipwa stahili zake liko pale pale, usihame kama hujalipwa pesa yote, hakuna atakayefukuzwa kwa kuwa amekataa kuhama kwa sababu hajalipwa pesa yake." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Kwa walimu na wanafunzi mnapomaliza masomo mkubali kufanya kazi katika vituo mnavyopangiwa, itafika mahali mwalimu akikataa kufanya kazi kwenye kituo alichopangiwa tutamfukuza, ni lazima kukubali kufanya kazi popote." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Tunataka kuwa na hifadhi za jamii mbili, moja kwa ajili ya kushughulikia sekta binafsi na nyingine watumishi wa serikali, lakini ukweli ni kwamba NSSF itabaki kama ilivyo, sema nyingine zote zitashughulikia watumishi wa Umma." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Tunapoziunganisha hifadhi hizo lengo letu ni kuboresha maslahi ya wafanyakazi na wanachama hivyo ondoeni hofu kabisa, sio lengo la serikali kuwanyima raha wafanyakazi wake wakiwemo waalimu." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Mimi kwenye Chama Cha Mapinduzi hata wakibaki watatu potelea mbali, lakini atakaye jihusisha na rushwa atashikwa bila kujali vyeo vyao, na tunawashika kweli, wengine hatuwatangazi, hata mimi nikifanya mimi rushwa, nitajishika mwenyewe." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
"Ilifika mahali jumuiya hii ya walimu ilikuwa inafanya kazi kama chombo cha siasa, msikubali, pia msikubali kuchagua viongozi kwa rushwa." – Rais John Magufuli
— AyoTV (@ayotv_) December 14, 2017
JPM: ”CCM hata wakibaki watatu, potelea mbali”
JPM ataka BoT kuacha matumizi ya Dola nchini