Wajasiliamali leo wakisherehekea mwaka mmoja wa Guta Vikoba Endelevu katika viwanja vya shule ya Msingi Bunju A, katika hafla hiyo iliyohuduriwa na mgeni rasmi afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Kinondoni Halima Kayeme kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo.
Wanachama wa Buta Vikoba Endelevu walipata nafasi ya kupata uhamasishwaji katika ujasiliamali kutoka kwa Dr Chriss Mahuki ambaye ni mwanasaikolojia na Maida Waziri ambaye ni Rais wa Wanawake Wajasiliamali Tanzania.
Katika hafla hiyo Buta pamoja na Mkurugenzi wao Semeni Gama ambaye amethibitisha kuwa Buta wanajumla ya vikundi 270 Tanzania nzima, licha ya kuzindua mradi wao wa Basi aina ya Coaster, Bajaj na Pikipiki katika kusherehekea mwaka mmoja wa Buta, walipata maneno ya uhamasishaji kutoka kwa Maida Waziri.
Maida Waziri kwa wasiomfahamu ana historia ya kusisimua katika kutafuta maendeleo na sasa amefanikiwa kuingia hadi katika rekodi za Afrika kwa jitihada zake ila lengo lake kuu ni kuwa tajiri namba moja wa kike Afrika.
Maida katika miaka yake 28 katika biashara amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo ya ukandarasi bora wa kike, ndio mwanamke wa kwanza kuwahi kumiliki boti ya uvuvi feli Dar es Salaam.
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga