Ni siku kadhaa tangu wafanyabiashara wadogo wadogo (Wamachinga) kuondolewa kando kando mwa barabara na kupelekwa kwenye maeneo yao husika yaliyotengwa na Serikali.
Najua nina watu wangu mnataka kufahamu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda atazungumza nini juu ya maeneo hayo husika….’Kwa upande wafanyabiashara ndugu zetu wamachinga hakuna Serikali yenye nia mbaya nao lakini tunachotafuta kuhakikisha mazingira au kutengeneza kila mmoja kufanya kazi katika maeneo yao maalum na sio tu wamachinga bali hata watu wengine’- Paul Makonda
‘Kwahiyo nawaambia kwamba hatuna nia mbaya na kule wanapokwenda tutaendelea kuhakikisha mazingira yao yatakuwa mazuri zaidi na zaidi, lakini ningependa kuwaambia watanzania waache tabia ya kununua vitu bila kuwa na risiti kwani ni muhimu kuwa na risiti ili baadae’ – Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA MUONEKANO WA BARABARA ZA K/KOO BAADA YA WAMACHINGA KUONDOLEWA ITAZAME HII VIDEO HAPA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE