Jumapili ya September 30 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam ulichezwa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga na game hiyo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare tasa.
Mchezo huo ambao huwa na presha pande zote, lilijitokeza tukio la kuwashangaza wengi kwa kiungo wa Simba raia wa Ghana James Kotei kumpiga mgongoni beki wa Yanga Gadiel Michael na tukio hilo kunaswa na camera za Azam TV.
Baada ya Kotei kuomba radhi na Gadiel Michael kuona ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa instagram, aliandika ujumbe wa kuashiria kuwa yameisha na hana kinyongo tena na Kotei.
“Asante sana kaka Kotei ombi lako la msamaha limekubaliwa heshima na upendo kwako, kilichotokea kimeshatokea, wote ni familia moja sasa acha tugange yajayo”
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga