Moja kati ya stori iliyowahi kutawala vichwa vya habari ni pamoja na hii ya Rais wa Marekani Donald Trump kupinga kauli ya mwandishi wa habari wa Brazil kusema kuwa Brazil wao ni bora katika soka duniani ukilinganisha na mataifa mengine.
Trump alinukuliwa akipinga kauli hiyo kwa kusema kuwa kama Brazil ingekuwa bora basi wasingeondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika nchini Urusi, Brazil ilitolewa na Ubelgiji katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa magoli 2-1, hivyo kwa ukubwa wa Brazil kuondolewa katika hatua ya robo fainali ni fedhea.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Tite akifanya mkutano na waandishi wa habari ameijibu kauli hiyo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kwa kumwambia Trump kabla ya kuikosoa Brazil anapaswa akumbuke rekodi yake katika michuano hiyo kuwa imewahi kutwaa World Cup mara tano (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002).
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe