Chama chaa soka Ulaya UEFA limetangaza rasmi kuanzisha mashindano mapya ya club nje ya UEFA Champions League ambayo tumeyazoea, UEFA wametangaza dhamira hiyo na kueleza lengo la mashindano hayo ambayo yatakuwa yanachezwa siku ya Alhamisi ni kuvipa fursa vilabu visivyopata nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa.
Mashindano hayo yatahusisha jumla ya timu 32 ambapo yatajumuisha timu mbalimbali kutoka madaraja mbalimbali, mashindano hayo ambayo yataanza kuchezwa 2021 yatajulikana kwa jina la UEL2 kwa kirefu ni UEFA European League 2, ambapo timu 32 zitagawanywa katika makundi nane.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa UEFA Mr Aleksander Ceferin inaeleza hivi “Mashindano mapya ya UEFA yatafanya mashindano ya club yavutie zaidi kuliko yalivyokuwa” Ujio wa mashindano hayo hauyaondoi mashindano yaliyopo ya club kama UEFA Champions League na UEFA Europa League bali lengo ni kuongeza mashindano ya club.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?