Kundi la mataifa tajiri duniani ya G7 wamefanya mkutano wa dharura kuhusu aina mpya ya kirusi cha Covid-19 ambacho kimebadilika kabisa kilichopewa jina la Omicron, ambacho kisambaa kwa kasi.
Kirusi hicho kimelazimisha mataifa kufunga mipaka yao, huku wataalamu wakiwa katika uchunguzi wa kina wa kutaka kujua athari zake katika jitihada za kukabiliana na janga.
Mkutano huo umeitishwa na Uingereza ambayo inashikilia kiti cha mataifa hayo lakini pia ni moja kati ya mataifa ambayo idadi kubwa ya athari za kirusi hiko imegundulika.
Kirusi Omicron ambacho kwa mara ya kwanza kiligundulika Afrika Kusini kinasababisha changamoto mpya ya jitihada ya ulimwengu katika kuliangamiza janga la Covid-19. Nchi kadhaa zimeweka vizuizi kwa hofu ya kwamba uenda hali mbaya ikajirudia.