Tangu Jumamosi, mapigano kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Al-Bourhane na vikosi vya kijeshi vya mshirika wake wa zamani, Jenerali Mohammed Hamdan Daglo, anayejulikana kama Hemetti, yamesababisha karibu watu 200 kuuawa na takriban 1,800 kujeruhiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Kutokana na hali hii, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa majenerali hao wawili kukomesha mara moja uhasama kwa sababu unaweza kuwa mbaya kwa nchi na kanda nzima.
Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 Jumanne tarehe 18 Aprili walitoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mapigano nchini Sudan
kupunguza mvutano na kurejesha utawala wa kiraia nchini Sudan, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi kubwa zilizoendelea kiviwanda wamesema baada ya kukutana nchini Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kwa upande wake, alizungumza kando siku ya Jumanne na majenerali hao wawili hasimu wanaopigania mamlaka nchini Sudan na kusisitiza “udharura wa kufikiwa kwa usitishaji mapigano”, kulingana na msemaji wake, Vedant Patel.
Kusitishwa kwa mapigano kutasaidia kutoa misaada ya kibinadamu kwa wale walioathiriwa na mapigano, kuunganisha familia za Sudan zilizotawanywa na mapigano na kuhakikisha usalama wa wanachama wa jumuiya ya kimataifa huko Khartoum”, kulingana na kauli ya Bw. Blinken iliyonukuliwa na na Bw. Patel katika taarifa.
Siku ya Jumatatu, msafara wa kidiplomasia wa Marekani kuelekea Sudan ulishambuliwa, lakini hakuna aliyejeruhiwa na siku hiyo hiyo, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo alishambuliwa nyumbani kwake.
Mapigano hayo yalizuka baada ya wiki kadhaa za mvutano wa kuwania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021. Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi chenye nguvu cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).
Umoja wa Mataifa umesitisha shughuli zake nyingi nchini humo, alisema msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, ambaye alisisitiza Umoja wa Mataifa hautakuwa na ulazima wa kuwahoji wahudumu wake wasipotokea maofisini kutokana na mashaka ya usalama.
Takriban watu 185 wameuawa na wengine 1,800 kujeruhiwa katika mapigano ambaye yanaendelea kwa muda wa siku nne sasa kati ya pande zinazohasimiana nchini Sudan. Hayo ni kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan.