Headlines za viongozi wa club ya Yanga kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya Yanga na kuiacha timu katika kipindi kigumu, ndio inaendelea kwa sasa, hivyo sintofahamu inazidi kutanda nini itakuwa hatma ya timu hiyo kuelekea msimu wa 2018/19.
Kutokana na matatizo na changamoto zinazoendelea katika club hiyo mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe ameandika maneno au ushauri katika page yake ya instagram ikilenga kuwakosoa wale mashabiki wa soka ambao wanapenda kuwakwaza wafadhili wa timu hizo.
“Pesa sio makalio kwamba kila mtu anayo……tujifunze kuheshimu watu wenye pesa..zile kelele za nyakati zile za watu fulani dhidi ya Manji..wakimpinga sana…wengine wakasema “Atuachie Yanga yetu”
“Leo ndo muda wao wa kuichukua Yanga yao, wakalipe Kambi, wawalipe akina Yondan na Kessy, washushe akina Kagere wao pale Jangwani Yaani Manji hayupo na hakuna atakayewakataza…yuko wapi yule Mzee? Yuko wapi yule kijana machachari?”
“Iliwahi kutokea pale Tanga..watu walimwambia Nassor Binslum awaachie timu yako..wakaishia kushuka na kupoteza dira…Simba iko Uturuki na kuna watu hawamtaki Mo..waambie wamsajili mchezaji mmoja tu kwa shilingi milioni kumi”
“Baada ya dakika tano ukiwapigia simu utasikia ‘Namba unayopiga haipatikani’…Pesa sio makalio kwamba kila mtu anayo…nadhani baada ya Yale yanayotokea Jangwani tutaanza kuheshimu wenye pesa…huu sio mpira wa nyakati za Ujamaa kwamba unamnunua Makumbi Juma kwa kumpa feni ya ukutani…tuheshimu wenye pesa!!! Asanteni”
USAJILI WA YONDANI: Manara asema “Mimi ndio msemaji wa SIMBA SC”