Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuuza hisa kwa umma itakayofuatiwa na kujiunga kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu kumilikisha asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Akizungumzia hatua hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Bwana Ian Ferrao alisema.
“Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na tumewasilisha maombi na utaratibu mzima utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima kuhusiana mchakato huu kwenye Mamlaka ya Usimamiaji wa Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa (DSE)”.
“Hatua hii ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la kuuza hisa zake kwa umma na inadhihirisha jinsi ilivyojipanga kuendelea kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni”
“Tunaamini uuzaji wa hisa zetu kwa umma utazidi kukuza shughuli za Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kunufaisha watanzania kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Kampuni yetu haitajulikana kwa jina la mwanzo la Vodacom Tanzania Limited bali itakuwa na jina laVodacom Tanzania Public Limited Company (Plc) ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kuingia sokoni.
Tunawahakikishia kuwa mchakato wakuingia kwenye hatua hii umeanza vizuri kwa mafanikio na tunaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini kuhakikisha tunatimiza dhamira ya kuanza kuuza hisa kwa wananchi yenye dira ya kuleta manufaa kwa wote.”
Ferrao alitoa msisitizo kuwa Vodacom inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hii inaleta manufaa kwa pande zote zinatazohusika kuanzia wanunuaji wa hisa, kuendelea kuwekeza, kuendelea kuleta mapinduzi ya ubunifu wa kiteknolojia na kuimarisha ubora wa huduma za kampuni kwa wateja wake
“Tutaendelea kutoa mchango mkubwa wa ufanikishaji wa sera ya nchi ya miaka 5 yakukuza sekta ya mawasiliano.Tutaendelea pia kuwaletea taarifa mbalimbali kuhusiana na mchakato wa kuuza hisa kwa umma unavyoendelea” – Ferrao.
Wengine kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, wanaoshuhudia kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. GeraseKamugisha, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wa pili kulia) na Mkuu wa fedha wa kampuni ya Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel (watatu kutoka kulia)
VIDEO: Alice Tupa anayo Magazeti yote ya leo November 28, 2016. Bonyez play kutazama hapa