Kama ni mfuatiliaji wa soka la Ligi Kuu England basi najua jina la mtangazaji wa michezo wa England Gary Lineker litakuwa sio geni masikioni kwako, kama ambavyo wengi walikuwa wakikaa na kusubiria kuanza kwa EPL basi wapo pia waliokuwa wanasubiria kumuona Lineker akitangaza TV Show yake ya kwanza ya EPL akiwa kavaa boxer.
Gary Lineker msimu uliopita wa Ligi Kuu England 2015/2016 wakati Leicester City wanatabiriwa na baadhi ya watu kuwa watatwaa Ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kufanya vizuri na kuvuna point katika michezo mingi, Lineker aligoma kuwa Leicester hawawezi kutwaa EPL na kama ikitokea wakifanya hivyo atafanya show yake akiwa na boxer.
Kwa bahati nzuri Leicester City walitwaa taji hilo na mwanzo wa mechi za ufunguzi za EPL August 13 2016, Gary Lineker alitekeleza ahadi hiyo kwa kufanya show yake ya kwanza ya ufunguzi wa EPL akiwa na boxer, kama utakuwa unakumbuka vizuri Lineker aliwahi kuichezea Leicester City kwa miaka 7 na kuhama timu hiyo 1985 na kujiunga na Everton.
Lineker ametimiza ahadi yake aliyoiweka kuwa Leicester wakitwaa ubingwa wa EPL atafanya show ya EPL akiwa na boxer. pic.twitter.com/izWJggqWZA
— millard ayo (@millardayo) August 13, 2016
GOAL AND HIGHLIGHTS: Yanga vs MO Bejaia August 13 2016, Full Time 1-0