Kiongozi mpya mwenye mamlaka nchini Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye alimpindua Ali Bongo Ondimba, ataapishwa kama “rais wa mpito” Jumatatu Septemba 4, 2023 mbele ya Mahakama ya Kikatiba, viongozi wa mapinduzi wametangaza kwenye televisheni siku ya Alhamisi Agosti 3.
Jenerali Oligui pia “ameamua juu ya kuanzishwa kwa taasisi za mpito”, ametangaza Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, msemaji wa Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi (CTRI), ambayo inawaleta pamoja makamanda wote wa jeshi.
Mbele ya mahakama ya kikatiba, Brice Clotaire Oligui Nguema, afisa wa ngazi ya juu katika jeshi aliyekomesha mamlaka ya zaidi ya miaka 50 ya familia ya Bongo nchini Gabon, “ataapishwa siku ya Jumatatu Septemba 4, 2023 kama rais wa Jamhuri” , mamlaka ya kijeshi katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni.
Miongoni mwa matangazo mengine yaliyotolewa tarehe 31 Agosti 2023 na msemaji wa CTRI, kuanzishwa upya kwa muda kwa Mahakama ya Kikatiba, uanzishwaji wa taasisi za mpito, na kurejeshwa kwa safari za ndani za ndege.
“Aidha, (Jenerali Oligui Nguema) anawaagiza Makatibu Wakuu wote, mabaraza ya mawaziri, wakurugenzi wakuu pamoja na wakuu wote wa huduma za serikali kuhakikisha mara moja uanzishaji wa kazi unaendelea kikamilifu na utendakazi wa huduma zote za umma. “