Mke wa rais aliyeondolewa madarakani nchini Gabon Ali Bongo Ondimba, amabye amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika ya kati mwishoni mwa Agosti, amefungwa jela, wakili wake amethibitisha.
Sylvia Bongo Ondimba Valentin, anayeshukiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma, alifungwa jela siku ya Jumatano, wakili wake Francois Zimeray amesema.
Mke wa Bongo alishtakiwa Septemba 28 kwa utakatishaji fedha na kughushi rekodi.
Sylvia Bongo amekuwa amekuwa akizuiliwa nyumbani katika mji mkuu, Libreville, tangu mapinduzi ya Agosti 30 yalionagusha utawala miaka 55 wa familia ya Bongo.
Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa zamani wa nchi na wapambe wake walighushi matokeo ya uchaguzi.
Wanamshutumu Sylvia Bongo na mwanawe, Nourredin Bongo Valentin, kwa kumdanganya rais huyo wa zamani, ambaye hajapona kabisa kutokana na kiharusi kikubwa alichokabiliwa nacho mwaka wa 2018.
Aidha wawili hao wanatuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa za umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.