Ni Octoba 5, 2023 ambapo Galco Insurance kushirikiana na shirika la bima la Zanzibar ‘Zanzibar Insurance’ wamezindua rasmi huduma ya bima ya TAKAFUL.
Bima hii ya TAKAFUL inaelezwa kuwa inafuata misingi ya Sharia za dini ya kiislamu lakini sio kwa ajili ya waamini wa dini ya kiislmu tu bali kwa watanzania na Wananchi wote wakaopendezwa kujiunga na bima hii.
Akizungumza CEO wa makampuni ya GSM, Mr Benson Mahenya alisema..‘Kampuni yetu ya Galco Insurance Brokers kama sehemu ya makampuni ya GSM, imeanzishwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa lengo kuu la kuwa kiunganishi kati ya wahitaji wa huduma za bima na makampuni ya bima”
“Huduma zetu za bima sio sera tu bali ni ahadi ya kuwa tupo karibu nawe pale utakapokutana na changamoto za kibiashara na kimaisha kwa ujumla, tunahakikisha unaweza kupitia dhoruba yoyote kwa kujiamini”- Alisema CEO wa makampuni ya GSM Mr Benson Mahenya