Ishu ya kuoa ni uamuzi wa mtu husika kuamua ni wakati gani anaona kwake unamfaa kufanya uamuzi huo ambapo kuna hii imetokea Kenya baada ya Gavana wa benki kuu ya Kenya Patrick Ngugi Njoroge kuzua mjadala wakati wa kikao cha kamati ya bunge na kutangaza kuwa bado hajaoa ingawa umri wake ni mkubwa.
Baada ya kuulizwa na wabunge kwa nini mpaka sasa hajaoa Gavana huyo ambaye kwa mwezi analipwa mshahara wa milioni 3 za Kenya ambazo kwa Tanzania zinagonga kwenye 67737395 alisema ni chaguo lake kuwa peke yake kwa kuwa hajakiuka maadili ya jamii kwa njia yoyote ile.
Muda mfupi baada ya kuweka hadharani kutokuwa na mke baadhi ya Wanawake walimiminika kwenye mitandao ya kijamii kutaka kupata nafasi hiyo ya kuolewa na Gavana na kama ilivyoripotiwa na Citizen TV Kenya.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.