Tamasha la Filamu la Kimataifa la Cannes linaanza leo May 8, 2018 huko nchini Ufaransa na mwaka huu zimetambulishwa sheria mpya zitakazotumika.
Moja ya sheria hizo mpya ni pamoja na marufuku ya kupiga picha binafsi yaani ‘selfie’ kwenye zulia jekundu.
Katika tukio hilo pia hakutakuwa na matangazo ya vyombo vya habari mbalimbali na hii ni tofauti na inavyofanyika kila mwaka.
Waandaaji wa tamasha hilo pia watashirikiana na serikali ya Ufaransa kubuni nambari za usaidizi kwa wanawake kuweza kuripoti visa vya unyanyasaji wa kingono.
Maswali matano makubwa yaliyoulizwa Bungeni May 8, 2018