Mkoa wa Kagera umepatiwa msaada wa Redio koo 20 na camera za angani 2 ili kusaidia zoezi linaloendelea mkoani humo la kuwaondoa wafugaji na mifugo yao katika mapori ya akiba na misitu ya hifadhi.
Msaada huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya huduma za ulinzi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Meja Jenerali Mstaafu Hamis Selufuko na kusema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha mawasiliano wakati shughuli ya operation ikiwa inaendelea maporini pamoja na kutumia camera za angani kuona wanyama na wafugaji ambao wapo maeneo yasio rahisi kufikika.
Mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na serikali amepokea vifaa hivyo na kusema kuwa wanaamini nguvu ya kufanikisha zoezi lao imefanikiwa. Full video nimekuwekea hapa chini tayari..
VIDEO: ‘Kijiji cha Koromije sivyo ambavyo watu wanavyofikiri’-Mbunge Susanne
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo