Jeshi la Israeli limedaiwa kushambulia hospitali katika ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 500, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.
Takriban majeruhi 350 kutoka Hospitali ya al-Ahli Arab walisafirishwa kwa haraka hadi katika kituo cha matibabu cha msingi cha Jiji la Gaza, Hospitali ya al-Shifa, ambayo tayari ilikuwa ikijitahidi kukabiliana na watu waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi yaliyotangulia ya Israel, mkurugenzi wake aliliambia Shirika la Habari la Associated Press. Mohammed Abu Selmia.
Wahasiriwa walifika wakiwa na majeraha mabaya, kama ilivyowasilishwa na Ashraf al-Qidra, msemaji wa wizara ya afya ya Palestina huko Gaza.
Majeraha haya yalijumuisha kukatwa kichwa, kukatwa matumbo, na kukosa miguu na mikono.
Wafanyakazi wa hospitali waliozidiwa walilazimika kuamua kufanya upasuaji kwenye sakafu na kwenye korido, mara nyingi bila ganzi.
Abu Selmia alisisitiza kwa haraka uhitaji mkubwa wa vifaa vya matibabu, dawa, vitanda, ganzi, na mambo mbalimbali muhimu.
Shambulio hili, limelaaniwa na viongozi wa nchi mbalimbali duniani, akiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye amesema hakuna sababu yoyote inayoruhusu hilo kufanyika.
Kilichojiri kimesababisha kufutwa kwa mkutano nchini Jordan, ambako rais Biden alikuwa akutane na viongozi wa nchi za Kiarabu.
Waziri Mkuu wa Israli Benjemin Netanyahu amekanusha kuhusika kwa jeshi la nchi yake kushambulia hospitali, akisema limetekelezwa na kundi la kijihadi katika ukanda wa Gaza, kundi ambalo limekanusha pia kuhusika.
Tangu kuanza kwa vita hivyo, Oktoba 7 baada ya kundi la Hamas kushambulia Israeli, Wapalestina zaidi ya 3,000 wameuwa kwenye ukanda wa Gaza huku Waisraeli zaidi ya 1,400 wakipoteza maisha.