Ripota wa AyoTV na millardayo.com wakati akiwa anasubiria mchezo wa fainali na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama AFCON U-17, amekusogezea mambo matano usiyoyafahamu kutoka Gabon.
1- Wote tumekuwa tukiamini au kuzoea kuona kuwa Taxi za Airport ni gari ambazo nzuri na wakati mwingine zinakuwa hata mpya husani kwa Tanzania kutokana na kuwa zinakuwa sehemu ambayo wageni kutoka nje ya nchini wanaingia, hiyo ni tofauti kwaGabon Taxi nyingi au gari zinazobeba abiria Gabon ni chakavu na gari mpya za watu binafsi.
3- Gabon ni nchi ambayo ina idadi ndogo ya watu milioni 1.8 ukilinganisha na Tanzaniaambayo ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 40, mji mkuu wa nchi hiyo ambao unajulikana kama Libreville ni mji ambao unajumla ya watu 578156 hiyo kwa mujibu wa takwimu 2017.
4- Kwa nchi ya Gabon wenye wanasema msichana yaani mwanafunzi akipata ujauzito wakati bado yupo shuleni hawezi kufukuzwa shule bali ataruhusiwa kuendelea na masomo huku akiwa bado mjamzito akikaribia kujifungua anapewa ruhusa ya uzazi na baadae anarudi kuendelea na masomo.
5- Staa wa soka mkubwa Gabon ni nahodha wao Pierre-Emerick Aubameyang ambaye anacheza Borussia Dortmund licha ya kuwa na jina kubwa Gabon hana makazi yaani huwa anakuja timu ya taifa na kuondoka, hiyo inatokana na kuzaliwa na kukulia Ufaransa, baba yake ana asili ya Gabon na mama yake ni mfaransa mwenye asili ya Hispania.
Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.