Kutoka nchini Msumbiji inaelezwa kuwa siku za hivi karibuni takriban watu 2,400 wamepoteza ajira na vibarua vyao kutokana na ugonjwa mpya unaoikabili nchi hiyo kwa sasa maarufu kama ugonjwa wa Panama.
Ugonjwa huo unatajwa kushambulia kwa kasi mazao ya ndizi na kusababisha biashara hiyo kulegalega na kufanya watu kupoteza kazi zao nchi zima, katika sekta zote zinazohusiana na mazao hayo.
Mamlaka nchini humo zimeeleza kuwa maambukizi hayo ya fangasi ambayo ndiyo yanasababisha ugonjwa huo wa Panama kwenye ndizi umeathiri mashamba makubwa ya ndizi kwenye majimbo ya Kaskazini mwa nchi hiyo ya Nampula, Cabo, Delgado kwa takriban ekari 1,300.
Mpaka sasa inatafutwa mbegu ya aina nyingine ya ndizi ili kwamba wafanye mbadala wa ndizi hizo zinazoathiriwa na ugonjwa.
Kuongezeka Bili ya maji Mkurugenzi azungumza “Maji ya DAWASCO ni bure”