Leo January 30, 2018 Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibarahim Hamis Juma amesema Mahakamani hakuna utajiri, hivyo vijana wanaotafuta ajira wasitegemee kutajirika.
Jaji Prof. Juma ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Feza, baada ya kutembelea Mahakama Kuu ya Tanzania na kuongeza kuwa Mahakama ni sehemu inayohitaji watu wenye umakini hasa kwa kuzingatia taaluma na nidhamu.
Amesema kuwa dunia ya sasa imekuwa na malalamiko kuhusu kushuka kwa maadili, hivyo maadili na taaluma ni vitu muhimu katika Jamii. Ameongeza kuwa suala la rushwa limekuwa changamoto katika jamii, hasa katika ajira ambapo pia jamii inashindwa kutoa taarifa kuhusu suala hilo.
“Hivyo kwa vijana mnaotarajia kutafuta ajira Mahakamani huku hakuna kutajirika, hivyo mkiingia katika ajira muepukane na rushwa.” Jaji Prof Juma
Watumishi wa Mahakama, wadau wa sheria kupata mafunzo Kidigitali….