Leo February 18, 2018 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia Askari Polisi sita kutokana na kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT Akwilina Maftah mwenye miaka 22.
Mambosasa amesema February 16, 2018 CHADEMA walifanya mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja vya Buibui Mwananyamala ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe alipanda jukwaani na kukatisha mkutano na kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kuandamana.
SACP Mambosasa amesema kuwa Jeshi limeunda timu ya Upelelezi ili kuchunguza chanzo cha kifo cha binti huyo.
“Katika uchunguzi huo tunawashikilia askari 6 kufuatia tukio hilo pia silaha zao zinachunguzwa ikiwa ni pamoja ni pamoja na kuzipeleka kwa wataalamu wa milipuko,”-Kamanda Mambosasa
Pia Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo linawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini kama miongoni mwao walikuwa na silaha za moto na linaendelea kuwatafuta wafuasi na Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki katika maandamano.
“Tunawashikilia Askari 6 ambao wametumia Silaha za moto katika Uchaguzi huu mdogo,”-Mambosasa.#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/BXBusRP70d
— millardayo (@millardayo_) February 18, 2018
“Tendo lililompata Binti ni la bahati mbaya sana, kwani wale Wawili waliojeruhiwa walikuwa eneo la tukio,”-Kamanda Mambosasa#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/2zqEhdOx6S
— millardayo (@millardayo_) February 18, 2018
IMETHIBITISHWA: “RISASI MOJA IMEMPATA MTU AMEFARIKI”