Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea kuwa na Maafisa Uvuvi ambao wanashirikiana na wahalifu kufanya vitendo vya hujuma wakati kuna vijana wengi wenye nia njema ya kulitumikia Taifa wanahangaika na ajira.
Gekul ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha kuchakata samaki, kilichopo Vingunguti jijini DSM Januari 5, 2021.
“Tulikuwa Kanda ya Ziwa na hapa pia kilio ni hicho hicho malighafi, malighafi zinapungua kwa sababu baadhi ya Maafisa uvuvi wanashiriki katika vitendo vya uvuvi haramu, wanashirikiana na wahalifu, hata pale ambapo vyombo vya ulinzi na usalama vinapotaka kufanya operesheni ya kuwakamata wahalifu wamekuwa wakitoa taarifa kwa wahalifu hao kama ambavyo ilitokea hivi karibuni kule Wilayani Babati” Gekul
“Kwa nini tuendelee na watu wa namna hii wakati kuna vijana wengi wenye nia njema na taifa lao wapo huko nje hawana ajira na huku ndani ya Serikali kuna baadhi ya watu wanahujumu taifa na uchumi wa nchi, hatuna haja kuendelea kuwa na watu kama hawa,” Gekul