Steven Gerrard ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al-Ettifaq inayoshiriki Ligi ya Saudia hadi 2027.
Al-Ettifaq kwa sasa wanashika nafasi ya nane kwenye jedwali, pointi 28 nyuma ya viongozi Al-Hilal.
Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool na England alisema: “Hili linanifurahisha sana mimi na familia yangu na ninahisi kama kutambuliwa kwa bidii na kujitolea.
“Tulilazimika kuweka miundombinu mipya, kama vile kujenga uwanja mpya wa mazoezi kwa awamu na kujenga uwanja mpya. Lakini mengi yamepatikana.”