Kiungo wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani Steven Gerrard yuko tayari kustaafu soka. Kiungo huyo ambaye alijiunga na klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwa mkataba wa miezi 18 ameweka bayana muda ambao huenda akastaafu soka.
Gerrard ambaye kwa sasa anacheza soka huku akiwa mchambuzi wa soka wa BT Sport ametangaza kuwa msimu ujao utakuwa wa mwisho kucheza soka, hivyo tutegemee kumuona Steven Gerrard akitangaza rasmi kustaafu soka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati ambao atakuwa na umri wa miaka 36 angeweza kuwa na uwezo wa kuendelea kucheza soka.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amewahi kucheza soka katika klabu mbili tu toka aanze kucheza soka, Gerrard alianza kucheza soka la katika timu ya wakubwa toka mwaka 1998 katika klabu ya Liverpool kabla ya mwaka 2015 alipoamua kuhamia klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwa mkataba wa miezi 18, hata hivyo timu ya Galaxy anayoichezea staa huyo ilitolewa wiki iliyopita katika mechi za play offs dhidi ya Seattle Sounders.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.