Kocha wa kijerumani ambaye ana muda wa wiki kadhaa toka ajiunge na Liverpool kama kocha mkuu wa klabu hiyo, baada ya uongozi wa Liverpool kumfuta kazi Brendan Rodgers. Ikiwa ni siku moja imepita toka kiungo mwenye heshima kubwa katika klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza Steven Gerrard athibitishe kuwa anafikiria kustaafu soka.
Baada ya siku ya November 3 Gerrard kuthibitisha kuwa huenda akastaafu soka mwishoni mwa mwaka 2016 kocha wa Liverpool Jurgen Klopp leo November 4 amethibitisha kuzungumza na Steven Gerrard na kuwa ana mpango wa kutaka kumrudisha kiungo huyo Anfield.
Awali kabla ya Brendan Rodgers hajafukuzwa aliwahi kumwambia Gerrard kuwa wakati atakapokuwa Uingereza kwa mapumziko aende kufanya mazoezi pamoja na Liverpool katika uwanja wao wa mazoezi wa timu hiyo Melwood ila stori za zilizotoka November 4 Jurgen Klopp kathibitisha kuongea na kiungo huyo kuhusu kurejea Liverpool klabu ambayo ndio alianza kucheza soka la ushindani.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.