Timu ya taifa ya Uganda imeondolewa rasmi katika michuano ya fainali za michuano ya mataifa ya Afrika 2019 AFCON, baada ya kuruhusu kufungwa kwa goli 1-0 dhidi ya Senegal na kuufanya mchezo wao wa 16 bora umalizika kwa 1-0.
Baada ya mchezo AyoTV ilimpata Emmanuel Okwi na kuzungumza nae kuhusiana na matokeo ya mchezo huo lakini kubwa ni kwa nini hapigi faulo kama anavyokuwa na club yake na kufunga na kumuachia Miya pekee? atacheza timu gani msimu ujao ngazi ya club?
“Namshukuru Mungu tumemaliza michezo yetu vizuri wachezaji wote wamepambana tumefanya kazi kwa pamoja, japo hatujaweza kuvuka sasa hivi mashindano yameisha tutajipanga tutajipanga upya, kuhusu faulo hayo ni maamuzi ya benchi la ufundi Miya pia ni mpigaji mzuri”>>> Okwi
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?