Walimu wa Shule ya Sekondari Bondeni iliyopo Arusha ,wamemfungia ndani ya ofisi Mkuu wa shule hiyo, Rahim Massawe Kwa kushindwa kushughulikia malimbikizo ya mishahara yao inayofikia kiasi cha zaidi ya Tsh 10 milioni kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo.
Wakizungumzia suala hilo waalimu hao wamesema kuwa, wamefikia hatua ya kufanya hivyo kama sehemu ya kushinikiza madai yao ya kulipwa malimbikizo ya mishahara yao ambayo wamekuwa wakiidai kwa kipindi kirefu bila mafanikio.
Mwalimu Rose Sechume amesema kuwa, shule hiyo hapo awali wakati ikiendeshwa na Bakwata mkoani hapa walikuwa wakilipwa mishahara yao bila shida yoyote ila tangu wameingia ubia na mwekezaji wa kampuni ya Zaim Education Development Ltd.
Aliendelea kusema baada ya mabadiliko hayo ambayo yalifanyika tangu Septemba mwaka huu mambo mengi yamekuwa hayaendi likiwemo suala la malipo yao.
Mkuu wa shule hiyo, Rahim Abbas Massawe ambaye amefungiwa ndani ya ofisi akizungumzia swala hilo kupitia dirisha la ofisi hiyo amesema kuwa, yeye binafsi aliwaita walimu hao ofisini kwake kuzungumzia swala hilo lakini hawajawahi kufikia muafaka.
Ulipitwa na hii? Waziri Jafo amsimamisha kazi Mkurugenzi