Moja ya habari iliyochukua headlines kwenye vyombo vya bahari barani Ulaya leo March 28, 2018 ni inayowahusu wanaume wawili wazee zaidi nchini Britain wanaotarajia kusherehekea kutimiza miaka 110 wiki hii.
Wazee hao ni pamoja na Robert Weighton ambaye alizaliwa Mjini Hull March 29, 1908 na Alf Smith ambaye ndiye mwanaume mzee zaidi nchini humo Britain.
Inaelezwa kuwa japokuwa wazee hao hawajawahi kukutana lakini wamekuwa wakitumiana kadi za birthday kutakiana heri kila wakisherehekea siku yao hiyo kwa miaka mingi sasa.
Wote wawili kwa nyakati tofauti wameeleza siri ya kuishi maisha marefu kuwa tabia ya kucheka ambayo inayosababisha mtu kuwa na furaha muda mwingi.
Weighton amenukuliwa akisema “kicheko ni kitu cha msingi sana. Matatizo mengi duniani yanatokana na watu kuwa serious sana muda wote”.
UFAFANUZI: Tanzania, Kenya hatiani kupasuka vipande viwili kujitenga na Afrika