Leo April 26, 2018 Kim Jong-un anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka Korea ya Kaskazini kuvuka mpaka na kuingia Korea kusini tangu kumalizika kwa vita ya wenyewe 1953, huku taratibu za mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki zikidaiwa kukamilika.
Rais wa Korea kusini Moon Jae-in anatarajiwa kumpokea rais mwenza Kim katika mpaka wa nchi hizo mbili majira ya saa 3:30 siku ya Ijumaa.
Mkutano huo wa kihistoria unategemewa kuzungumzia zaidi makubaliano ya Kaskazini iwapo amedhamiria kuachana na silaha za Nyuklia kama alivyotangaza hivi karibuni.
Mazungumzo hayo pia yamependekezwa kufanyika kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump, mapema mwezi June.
BREAKING: RAIS MAGUFULI ALIVYOIPANDISHA HADHI DODOMA KUWA JIJI