Imebainika kuwa mwili wa aliyekuwa mwanasiasa na mpiganiaji wa vyama vingi Kenneth Matiba wa nchini Kenya utachomwa leo April 27, 2018 badala ya kuzikwa.
Matiba anakuwa moja kati ya watu maarufu nchini Kenya ambao walitaka wachomwe na si kuzikwa kama ulivyo utamaduni wa nchi hiyo,
Kwa mujibu wa familia yake mwili wa Matiba utachomwa katika makaburi ya Langata.
Mbunge Lema amekamatwa na Polisi Arusha
Jambo hili limezua mjadala nchini humo, watu wakitaka kujua sababu halisi za maamuzi hayo, ambazo baadhi yake zimetajwa kuwa pamoja na gharama ya kuchomwa ni chini kuliko ile ya kuzikwa, changamoto ya nafasi za makaburi, inatajwa kuwa njia rahisi, wasiwasi wa kimazingira pamoja na masuala ya imani.
LIVE: TAKUKURU Temeke wanazunguza na waandishi wa habari