Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakamata watu watatu waliojitambulisha kama maafisa kutoka Ofisi ya Rais na kuchukua rushwa kwa mfanyabiashara wa madini.
TAKUKURU wilaya ya Temeke imeeleza kuwa waliweka mtego mnamo January 30, 2018 ili kuwanasa watu hao na walifanikiwa kuwanasa wakiomba rushwa.
Waliokamatwa ni Emmanuel Steven Kobelo anayejulikana pia kwa jina la James Afisa Mtendaji kata ya Jangwani, Julius Fredrick Chilumba, mfanyabiashara wa masuala ya bima, na Joseph Philip Chiluba Afisa Magereza Mstaafu.
Waliwakamata wakichukua rushwa na Tsh Milioni 2 kati ya Tsh Milioni 3 waliokuwa wameiomba ili kwamba wasimchukulie hatua mfanyabiashara mmoja ambaye alikuwa anashirikiana na wafanyabiashara haramu wa madini ya dhahabu na almasi.
BREAKING: ‘Sijanunuliwa na CCM, Kwani wakati najiunga na CHADEMA walininunua sh ngapi’