Upande wa Mashtaka umetakiwa kuifuta kesi ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani mil.6 inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA,Harry Kitilya na wenzake ambao ni aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon kwa sababu ya kucheleweshwa kwa vielelezo vya ushahidi kutoka nje ya nchi.
Ombi la kutaka kuondolewa kwa mashtaka hayo yametolewa na Wakili wa utetezi, Majura Magafu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa. Kabla ya ombi hilo Wakili wa Serikali, Pius Hilla alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wanaendelea kusubiri vielelezo vya ushahidi kutoa nje ya nchi.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi October 20,2017, huku akiutaka upande wa mashtaka uje na taarifa kamili katika tarehe hiyo.
Ulipitwa na hii? KESI YA MADINI YA ALMASI: Mahakamani tena leo