Taarifa zilizotufkia muda huu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, ni kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamis Kigwangalla amefanya uteuzi wa wajumbe wengine 8 watakaoungana na wajumbe wengine 23 aliowateua awali kuunda kamati ya kitaifa ya kuandaa mwezi maalumu wa Maadhimisho ya Urithi wa Tanzania.
Kati ya walioteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja mwanamitindo Jokate Mwegelo na muigizaji wa bongo movie Wema Sepetu ambaye hivi karibuni alitangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA.
Inaelezwa kuwa lengo kuu la mwezi huu maalumu ni kunadi utamaduni wa Kitanzania ndani na nje ya mipaka ya nchi ambapo kila kitu kitakuwa cha Kitanzania ikiwa ni pamoja na chakula, michezo, mavazi na ngoma za kiasili na mengineyo.
Pia imeelezwa kuwa mwezi huu utakuwa fursa ya kutangaza na kukuza utalii wa ndani. Wafuatao ni wajumbe wapya nane walioteuliwa,
- Anthony Mtaka Mjumbe
- Dr. Omar Abdulla Adam Mjumbe
- Ramadhani Ali Mchano Mjumbe
- Abdulla Khamis Ali Mjumbe
- Mussa Ameir Vuai Mjumbe
- Jokate Mwegelo Mjumbe
- Wema Sepetu Mjumbe
Barabara ya Pamba Mwanza itajengwa kwa Bil. 1, itafumuliwa upya.