Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amekatisha safari yake ya kushiriki kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola nchini Uingereza ili kukabiliana na maandamano na ghasia zilizolikumba Jimbo la Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo.
Katika mkutano, Rais Ramaphosa alitumia muda wake mwingi kujaribu kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kuwekeza nchini mwake, huku ikiwa ni safari yake yake ya kwanza ya kimataifa baada ya kutwaa madaraka hayo kutoka kwa rais mstaafu Jacob Zuma.
Ramaphosa amerejea nchini kwake kutokana na kuongezeka kwa ghasia na maandamano yanayodaiwa fursa za ajira, makazi pamoja na kuitaka serikali kukomesha rushwa inayodaiwa kukithiri nchini humo.
Ghasia hizo zimesababisha barabara kufungwa, magari kuchomwa moto na maduka yanavunjwa hovyo huku wakazi wa eneo hilo wakimtaka kiongozi wa jimbo hilo kujiuzulu.