Wataakam wa Afya kutokea Marekani wametembelea hospitali ya taifa ya Muhimbili na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya.
Ugeni wa wataalam tisa uliongozwa na mke wa balozi mstaafu wa Marekani Dr Deborah Stith ambaye amekiri kuwa wapo tayari kushirikiana na Muhimbili kwa karibu, huku akiongozana pia na madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti.
“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” >>>Prof. Lawrence
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe