Baada ya Dar es salaam Young Africans kutolewa katika hatua ya mtoano wa michuano ya club Bingwa Africa na Township Rollers ya Botswana, waliangukia katika michuano ya Kombe la CAF na kupangwa kucheza na Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli ya Yanga yakifungwa na Rafael Daudi dakika ya 1 na Emmanuel Martin dakika ya 54, nahodha wao Nadir Haroub mara nyingi siku hizi amekuwa hana nafasi ya kucheza baada ya dakika 90 aliongea na AyoTV na mikakati yake kwa ujumla.
“Nafasi ya kufuzu ipo sana kama tu tutatumia akili na kumsikiliza mwalimu ila tu nadhani Yanga tukiwa ugenini tunatulia na tunacheza vizuri sana cha msingi kuwasikiliza walimu, hapana timu yetu tunaangalia sana vijana ikitokea tatizo ndio kama hivi naingia kucheza lakini sio kama sina uwezo wa kucheza, siwezi kucheza zaidi ya Yanga hapa ni nyumbani baada ya hapo nitakuwa kocha”>>>Canavaro
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL