Staa wa zamani wa Club ya Arsenal na FC Barcelona Thierry Henry amezidi kudhihirisha kuwa maisha ya soka yana hatua zake na anaishi kulingana na mazingira, Herny kipindi anafanya kazi kama mchambuzi wa michezo Sky Sports alikuwa akionekana mtu mwenye mzaha sana lakini sasa hivi yuko tofauti.
Herny kwa sasa ni kocha wa AS Monaco ya Ufaransa na amekuwa sio mtu mwenye kupenda mzaha tena hata katika vitu vidogo, tofauti na ilivyokuwa awali alipokuwa akipenda kuleta utani katika kazi yake ya uchambuzi, kuelekea mchezo wao wa UEFA Champions League kati ya AS Monaco dhidi ya Borussia Dortmund amezichukua headlines wakati wa press conference.
Baada ya mkutano na waandishi wa habari katika chumba cha mikutano Henry akiwa kaambatana na golikipa Loic Badiashile mwenye umri wa miaka 20, alionesha kumuonya kutokana na mchezaji huyo kutorudisha kiti kama kilivyokuwa baada ya kumalizka mkutano huo, Monaco wanakamilisha ratiba lakini walishatolewa Champions League.
Thierry #Henry vs #Badiashile et sa chaise 👀😬#LateFC #ASMBVB #UCL pic.twitter.com/TzZI6tKXSw
— Late Football Club (@LateFootClub) December 10, 2018
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe