Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameamua kuendelea kuwa muumini wa wachezaji wenye nidhamu katika kikosi chake cha Yanga.
Zahera ambaye amekuwa akisifika kwa kuwa na misimamo migumu ili kulinda nidhamu na umoja katika timu yake, ametangaza rasmi kumvua unahodha wa Yanga Kelvin Yondani kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Kufuatia kitendo chake cha kuchelewa kufika mazoezini baada ya wachezaji kupewa siku tano za mapumziko na yeye kuja siku inayofuatia bila kutoa taarifa kwa kiongozi yoyote, Zahera ametangaza rasmi kumvua unahodha wa timu hiyo Kelvin Yondani na kumpa Ibrahim Ajib, hivyo kuanzia sasa Yondani ni mchezaji wa kawaida tu.
Kocha wa Simba baada ya kuwasili Zanzibar”Sio njia bora ya kuandaa timu”